Mtu mmoja amekufa na wengine wanne kujeruhiwa mjini Tukuyu wilayani hapa, baada ya radi kuupiga mti uliokuwa karibu na banda walipojihifadhi wakati mvua ikinyesha.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita karibu na vituo viwili vya mabasi ya daladala na yaendayo mikoani kandokando ya Barabara ya Mbeya-Malawi.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chalya Nyangidu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana na kwamba aliyefariki dunia ni mkazi wa jijini Arusha, Freeman Swai (35) ambaye alifika mkoani hapa kununua ndizi.
Waliojeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Makandana ni Oliva Ipyana (45), Anna Jericho (30), Juliana Francis (32) na Stela Nsile (37) wakazi wa wilayani hapa.
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Marco Mbata alithibitisha kupokea mwili wa Swai na majeruhi wanne. Alisema baada ya uchunguzi ilibainika, Swai aliungua kwa moto wa radi na kusaidiana na simu iliyokuwa ikitumia kupiga muziki.
Sunday, January 29, 2017
8:27 PM
Unknown
News
No comments
Related Posts:
MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA QT 2016/2017 HAYA HAPA | VIJANANAINJILI BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO … Read More
ASKOFU GWAJIMA AMJIBU MAKONDA KWA NAMNA YAKESaa chache baada ya kutakiwa kufika polisi na mkuu wa mkoa Paul Makonda kutoa taarifa juu ya madawa ya kulevya,Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima Amepost Ujumbe picha huu ambao wataalamu wa mambo wanada… Read More
UDOM: AILEN NICHORAS TOKA UDOM KUZINDUA ALBAM YAKE MPYA JUMAPILI HII (5/2/2017) |SITAKI KUKUMBUKA| AKISINDIKIZWA NA NYELANYELA NA STEWART UZINDUZI UZINDUZI UZINDUZI AMBAO HUJAWAITOKEA NI MWANADADA MWIMBAJI AILEN NICHORAS ANAKULETEA ALBAM YAKE YA KWANZA INAYOKWENDA KWA JINA LA SITAKI KUKUMBUKA HATA KUWA PEKE YAKE ATAAMBATANA N… Read More
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE(FORM FOUR) NA QT | BOFYA HII LINK UYATAZAME BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016… Read More
NA HIZI NDIZO SHULE VINALA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA WANAFUNZI VINARABaraza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne (CSEE) na QT kwa mwaka 2016. Jumla ya watahiniwa 277,283 ambao ni sawa na asilimia 70.09 ya watahiniwa waliofanya mitihani kidato cha nne 2… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment