JESHI la polisi Mkoani Mbeya,
linamshikilia mfanyabiashara
maarufu Jijini Mbeya, Steven
Samweli maarufu kwa jina la
MARANATHA, kwa tuhuma za
kujihusisha na biashara za
dawa za kulevya.
Maranatha ni mfanyabiashara
mkubwa Jijini Mbeya
akijijengea jina kubwa
kutokana na kumiliki
Pharmacy kubwa iliyopo
maeneo ya Kabwe,Jiji Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Dhahiri Kidavashari
alisema kuwa Maranatha,
alikamatwa juzi, kwenye moja
ya duka lake la biashara za
dawa baridi kwa matumizi ya
binadamu.
Alisema, baada ya polisi
kupata taarifa za kuhusishwa
kwa mfanyabiashara huyo na
mtandao wa dawa za kulevya,
liliweka mtego na hatimaye
kufanikiwa kumtia nguvuni na
sasa anahojiwa.
Aidha, kukamatwa kwa
mfanyabiashara huyo,
kunafikisha idadi ya watu
nane wanao tuhumiwa
kujihusisha na uingizaji,
usambazaji na utumiaji wa
dawa za kulevya Mkoa wa
Mbeya, huku watumiaji
wanaoshikiliwa wakiwa ni 23.
Mwisho.
Tuesday, February 21, 2017
11:15 PM
Unknown
News
No comments
Related Posts:
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AMANI MWASOTE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi. Mwasote, ambaye ni mwimbaji … Read More
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO TAREHE 11 APRIL 2017 |V.I.TZ … Read More
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO TAREHE 9/4/2017 |V.I.TZ LEO IKIWA NI SIKU YA TAREHE 9 may 2017 jumapili VIJANA NA INJILI TUNAWALEA MAGAZETI YOTE YA TANZANIA SOMA UPATE TAARIFA,MATUKIO NA HABARI ILI UPATE MAARIFA NA UFAHAM WA TAIA LAKO NA MATAIFA MENGNE YAKO … Read More
YAMETIMIA MADAM FROLA MBASHA KUFANYA BONGE LA HARUSI NA ATAZINDUA ALBAM NA KITABU CHA SIRI ZAKE Hayawi Hayawi sasa yamekuwa,lile tukio kubwa kabisa lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wengihatimaye siku imewadia.Si kingine bali ni harusi ya mwimbaji mahiri wanyimbo za injili kutoka nchini Tanzaniaanayefahamika k… Read More
V.I.TZ | HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO 12/4/2017 BOFYA HAPA KUTAZAMAGood Morning my people, today is 12 April 2017 and as usual my daily morning I give big news on the pages of newspapers from the Beginning and End of the Retort, Hardnews and Sports to find out what is going on my man do not … Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment