Na Ibrahim Yassin, Kyela
MKAZI wa Kitongoji cha Njisi,
Kijijiji cha Kilwa, wilayani Kyela,
Tummanye Makula (35) , amekaa
na ujauzito miezi 13 na
kushindwa kujifungua.
Hata hivyo, baada ya maombezi,
alijikuta akijifungua chura na
baadaye mdudu wa ajabu akiwa
na manyoya meusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa
wiki baada ya dada huyo
kumpigia simu Mchungaji wa
Kanisa la Tample Of Prayer For
All Nations Church, Nabii Charles
Mkuvasa wa mjini Kyela akihitaji
kuombewa.
Alicuhukua hatua hiyo baada ya
kukaa na ujauzito kwa muda wote
huo na kushindwa kujifungua,
licha ya kuzunguka kwa waganga
wa kienyeji.
Akizungumza na MTANZANIA
jana, Tummanye alisema
aliachana na mume wake muda
mrefu na kuamua kuishi na
mama yake mzazi.
Alisema baada ya miaka miwili,
alipata mwanaume mwingine
ambaye alimpa ujauzito huo na
siku zote alikuwa akihudhuria
kliniki katika Hospitali ya Wilaya
Kyela.
Alisema ilipofika miezi tisa,
alipata uchungu siku mbili, lakini
hakujifungua huku madaktari
wakimweleza kuwa njia yake ni
ndogo, licha ya kuwahi kuzaa
mtoto mmoja.
Baada ya siku mbili uchungu huo
ulikata na aliendelea kukaa na
ujauzito wake hadi alipoamua
kunywa dawa na kupiga lamri
kwa waganga wa kienyeji, ingawa
pia hakufanikiwa lolote, alisema.
Alisema alipokuwa nyumbani
aliambiwa na marafiki zake
aende kwa Nabii Charles
akaombewe kutokana na
kutokuwa na uwezo wa kutembea
na yeye aliomba namba ya simu
na kumpigia.
Alisema Charles alianza
kumuombea na baada ya dakika
tano, alisikia uchungu ikabidi
aingie ndani…muda mfupi
alijifungua chura ambaye
alitoweka katika mazingira ya
utata.
“Nilitoka sebuleni na kumweleza
mchungaji na mama yaangu
nimejifungua chura ambaye
ametoweka katika mazingira ya
utatanishi,” alisema.
Alisema baada ya muda mfupi,
alijisikia uchungu tena na kwenda
chumbani na kujikuta akijifungua
mdudu wa ajabu akiwa na
manyoya kama paka na nywele za
rasta, ikabidi amwite mama yake
na mchungaji.
Mama mzazi wa Tummanye
Makula hakuweza kutaja jina
wala kusema chochote, baada ya
gazeti hili kufika nyumbani
kwake, isipokuwa alikuwa akilia
tu muda wote.
Mkazi wa Kyela, Bonifas Mwalila,
mmoja wa mashuhuda wa tukio
hilo, alisema tukio hilo ni la
kwanza kuliona tangu azaliwe.
Naye Mchungaji Mkuvasa, alisema
baada ya kufika kijijini alimkuta
mama huyo akiwa katika hali
mbaya, kifo kilikuwa kinamwita
lakini kutokana na maombi
alimnusuru.
Diwani wa Kata hiyo, Anna
Makula licha ya kukiri kuwapo
tukio hilo, alisema amekuwa
akishuhudia matukio mengi ya
watu kufika kanisani hapo
wakiwa wamefungwa kamba,
lakini baada ya siku tatu alikuwa
akishangaa wakirudi makwao
wakiwa wazima.
Chanzo:Mtanzania
Monday, February 13, 2017
11:27 PM
Unknown
News
No comments
Related Posts:
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AMANI MWASOTE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi. Mwasote, ambaye ni mwimbaji … Read More
UDOM; EMMANUEL NYELANYELA KUZINDUA ALBAM YAKE MPYA TAREHE 7/5/2017 | V.I.TZ UZINDUZI WA ALBAM HII YA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ALIMAARUFU KWA JINA LA NYELANYELA Utafanyika tarehe 7/5/2017 ataambatana na waimbaji wengi sana baadhi yao wametajwa hapo juu AMBATANA NASI MPAKA SIKU YA TUKIO … Read More
MBEYA; UKWELI KUHUSU MZEE MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI AISHIE MBEYA TZ | V.I.TZBINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA. Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikiria Rekodi ya kula Chumvi ny… Read More
KIONGOZI WA MAKIRIKIRI AOKOKA|V.I.TZKiongozi wa kundi maarufu la Nyimbo za Asili la Makhirikhiri la nchini Botswana, Mosesi Malapela a.k.a Shumba Ratshega, ametangaza kumrudia Mungu baada ya kuokoka na kuanza kuhubiri neno la wokovu. Habari za uhakika kutoka kw… Read More
UDOM: MUSA MPUME KUZINDUA ALBAM YAKE 23/4/2017 | V.I.TZIn habari njema zenye furaha teleee KIJANA WA UDOM MUSA MPUME (DAKTARI MWIMBAJI) anatarajia kufanya uzinduzi WA Album yake ya kwanza tarehe 23/4/2017 jumapili Mahali tukio litakapofanyika ni CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM) K… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment