Sunday, January 15, 2017




Wapendwa nawasalimu katika jina la Bwana wetu mpendwa Yesu kirsto.
Karibu sana katika masomo ambayo utakuwa ukiyakuta katika ukurasa huu, Mungu akubariki sana.
Usisahau pia kumuhita Roho mtakatifu uendelee kutafakari nae somo hili na mengine yatakayo fuata baada hili.
pia ushauri wako ni muhumu sana ili kuboresha huduma hii kwako na MUNGU afanyike baraka katika maisha yako.


SOMO:UWAKILI


UTANGULIZI
Uwakili ni ile hali ya kufanya kazi au wajibu ulio pewa kwa uaminifu bila udanganyifu wowote, kwa maelezo hayo mafupi basi tunaweza kuona kuwa wakili ni mtu aliye chini ya sheria na anaye timiza wajibu wake kwa usahihi bila kufanya udanganyifu wowote.

Luka 12∶42➖44 Inasema., " Ni nani basi aliye wakili mwaminifu mwenye busara ambaye bwana wake atamuweka juu ya utumishi wake wote awape watu posho kwa wakati wake❓ heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta atamkuta anafanya hivyo, kweli atamweka juu ya vitu vyake vyote"

Kanisa leo liko katika hali ya uhitaji na umaskini kwasababu halija gundua ya kwamba siri ya kuondokana na hayo mambo ya uhitaji na umaskini ambao umekuwa wimbo wa taifa yampasa kila mtu kuwa wakili mwaminifu basi hapo ndipo kanisa na taifa kwa ujumla litapona.

Mtu anaweza kujiuliza kuna uhusiano gani kati ya uhitaji na umaskini kwa upande mmoja kwa kutokuwa wakili mwaminifu kwa upande mwingine,
kwa mtu aliye jiuliza swali kama hilo ningependa kumpa jibu kuwa kuna uhusiano mkubwa baina ya mambo haya ukitaka kuondokana na umaskini na uhitaji basi kuwa wakili mwaminifu, hilo ndo jambo la msingi linalo weza kukuvusha.

Inashangaza sana unakuta Wakristo hawatoi zaka kanisani na labda wengine walikuwa wanatoa ila kwasababu zisizo julikana wameacha. Nasema sababu zisizo julikana maana hakuna sababu maharumu kabisa ya kukufanya usimtolee Mungu zaka ikiwa nawewe unajihesabu kuwa ni wakili mwaminifu.
Pia mwingine anaweza kusema mahubiri ya namna hii ni mahubiri ambayo yamelenga baraka za kimwili tu na siyo za rohoni❗❗      Watu wa jinsi hii naomba niwajibu kuwa Injili ya Yesu ni Injili iliyo kamilika, ina uwezo wa kuhudumia roho, nafsi na mwili wa mwanadamu. si kweli kwamba Mungu hujishughulisha na roho zetu pekee na kwamba hajali kuhusu miili.
Mungu wetu utulinda na kututunza na kutufundisha mwili na roho ndipo baraka za Mungu hupitia ndiyo maana tunahitaji kuwa mawakili waaminifu kwake.



BAADA YA UTANGULIZI BASI TURUDI KATIKA SOMO LETU
Katika agano jipya wakili wajibu wake ni kumtolea bwana wake hesabu ama maelezo kamili juu ya jinsi alivyo timiza wajibu wake. kutokana na hili wakili sharti awe ni mtu mwaminifu ndiyo maana Bwana Yesu katika mistari ya LUKA,12∶42➖44 tuliyo isoma hapo juu anauliza ni nani aliye wakili mwaminifu ambaye bwana wake atamkuta akitimiza yale aliyo agizwa na bwana wake hapo bwana wake atakapo rudi?

Wakristo ni mawakili wa Mungu ambao Bwana Yesu amewaweka ili kuangalia mambo ya Mungu hapa duniani hivyo basi wakristo tuna wajibika kutoa hesabu au maelezo kamili kwa mambo yote yale ambayo Mungu ametupa, pia tuna wajibika na kuliangalia kanisa la Bwana maana wakili siyo mwenye mali bali anawajibika kwa wenye mali.

katika  Luka,16:1➖2 
"Tena aliwaambia wanafunzi wake, palikuwa na mtu mmoja tajiri aliye kuwa na wakili wake huyu alishtakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake, akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayo isikia juu yako? toa hesabu ya uwakili wako kwakuwa huwezi kuwa wakili tena."

Na katika 1kor,4:2 imeandikwa
"Hapo tena inayohitajiwa katika mawili ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu"
Hapo ndipo utaona jinsi gani uaminifu wa hali ya juu unahitajika ili uwe wakili mwaminifu.

pia mistari ifuatayo uhusiana na uwakili na uaminifu
  • Luka,12:42 "Bwana akasema ni nani basi aliye wakili mwaminifu mwenye busara ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?"


  • Mwanzo,1:28➖30 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema tazama nimewapa kila mche utoao mbegu ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti ambao matunda yake yana mbegu vitakuwa ndivyo chakula chenu, na chakula cha kila mnyama wa nchi na cha kila ndege wa angani na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi chenye uhai, majani yote ya miche ndiyo chakula chenu ikawa hivyo"


  • Wakolosai,1:25 "Ambalo nimefanywa muhudumu wake sawasawa na uwakili wa Mungu niliyo pewa kwa faida yenu nilitimize neno la Mungu"

MAENEO YA UWAKILI
Mungu ametupa maeneo ambayo tunatakiwa kuwa mawakili na waaminifu kwayo, maeneo hayo ni haya yafuatayo:

  1. MUDA:
  2. VIPAWA VYETU NA KARAMA
  3. HAZINA ZETU                                                                                                                                                                   
MUDA: Muda ni mtaji yulio pewa na Mungu ili tuutumie vizuri. naweza kusema kuwa muda ni mtaji muhimu sana kwa mwanadamu zaidi ya mtaji wowote ule, tofauti kati ya maskini na tajiri ipo kati  ya jinsi wanavyo tumia muda kila mmoja wao.
unaweza kuta mtu anasema aah, nipo tu hapa napoteza muda kweli ukiona ume kubari na kukiri kuwa unapoteza muda basi jua upo unajifilisi mwenyewe nivyema usipoteze muda.
Biblia inatufundisha kuutumia muda wetu vyema ZAB.90:12 "Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wa hekima" 
WAEFESO,5:15➖16 "Basi angalieni sana jinsi mnavyo enenda si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima mkiukomboa wakati kwamaana zamani hizi niza wokovu"

Ndugu wekeza muda wako katika vitu na mambo ya maana yanayo dumu milele, kuna mambo yasiyo dumu na kuna mambo yanayo dumu milele, nakushauri wekeza muda wako katika mambo yadumuyo milele.
Mfano wa mambo yadumuyo milele ni:
  • Neno la Mungu, tumia muda wako kusoma na kujifunza neno la Mungu.
  • maombi, tumia muda wako katika maombi
  • kazi ya Mungu,  n.k                                                                                                                                                                      

VIPAWA VYETU NA KARAMA: Hapa nina maana ya vitu binafsi alivyo tupan Mungu wetu mfano, Mwili, Ujuzi, Hekima n.k
USIMWUE FARASI KABLA HAJAFIKISHA UJUMBE, Unaweza kujiuliza kwamba labda nina maana gani kutumia huu msemo, ila maana yangu nikwamba Mungu ametupa vipawa mbalimbali vivyo tuvitumie kuwa mawakili waaminifu katika kipindi Mungu alicho tupa tuishi duniani.
Esta alitumia nafasi aliyokuwa nayo kuwaokoa Israel, pia Yusuph alitumia nafasi aliyo kuwa nayo katika jamii kuwasaidia ndugu zake waliokuwa hawana chakula,
hivyo yatupasa kutambua tumepewa karama kwa kusudi la kuvusha wasio weza kuvuka wenyewe
1korintho,12:4➖7"Basi pana tofauti za karama bali roho ni yeye yule, tena pana tofauti za huduma bali Bwana ni yeye yule, kisha kuna tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote, lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kusaidiana"



HAZINA ZETU:Ndugu uwe maskini au tajiri inabidi kuelewa kanuni za baraka zifuatazo:
  • Kanuni ya kurejeshewa: Luka 6:38,  Mithari,11:24➖31,  Zaburi,41:1➖3
  • Kanuni za kuringanisha kiwango na kipato: Luka,21:1➖4
  • Kanuni ya kutoa kwa moyo wa furaha: 2kor,9:7
  • Kanuni ya kupokea kutoka kwa wengine pale unapo kuwa muhitaji: 2kor,8:15

FEDHA
Naomba ujitahidi twende pamoja kabisa katika kipengele hiki maana tunahitaji kuwa mawakili waaminifu.
Kuna kanuni za Mungu za kukufanya uwe wakili mwaminifu kwa habari ya fedha, nazo ni hizi zifuatazo:
  • Uitunze na kuijari familia yako: 1tim,5:8
  • usiwe mpenda fedha: 1tim,6:10
  • Toa kwa kadri ya ulivyo navyo: 2kor,8:2
  • Utoaji wako utokane na kuongozwa na Roho mtakatifu na uwe una misingi ya Biblia: 2kor,9:7
  • Uwe mkarimu: 1yoh,3:17


ZAKA
BWANA anaagiza tutoe zaka Lawi,27:30ー33  pia tutoe malimbuko, Mithali,3:9
Katika agano jipya Bwana Yesu aliagiza hivi,: "Lakini ole wenu mafarisayo kwakuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga na huku mwaacha mambo ya adili na upendo wa Mungu iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza bila kuyaacha hayo ya pili" LUKA,11:42

KANUNI ZA ZAKA
10% ya mapato yako kabla ya makato yoyote ni zaka ya kumtolea Mungu,  zaka katika agano la kale lilitumika kuwatunza maskini na wahitaji katika Israel Kutoka,23:11 
Agano jipya kuwatunza maskini mdo,4:34一37, Rum,15:26ㅡ27  kuwatunza wahubiri na waalimu galatia,6:6, Luka,10:7

KUMBUKA
Sisi ndiyo tunao amua tuabarikiwe kwa kiasi gani Luka,6:38, mal,3:7─10, mdo,20:35
Unacho panda ndicho unacho vuna Galatia,6:7
Kutumia mali zetu kwa ajiri ya Mungu ni kuwekeza Luka,12:33
Mungu ndiye akupaye nguvu ya kutajilika Kumb,8:18
Mungu ndiye mwenye mali zote na vitu vyote ni vyake Zab.24:1




HITIMISHO
Habakuki,3:2
Ndugu tukumbuke kuwa fadhiri za MUNGU ni nyingi mno hasa pale tunapo tambua kuwa tumejikwaa na kutubu kwa iman basi Mungu hutusamehe na kuturudisha kundini, labda unamwitaji Mungu afufue utoaji wako basi nenda kwa unyenyekevu mbele zake nae ni mwaminifu na mwingi wa rehema atakusikia na kukujibu na kukusamehe pale utakapo kuwa umeteleza na kukupa kibali cha kuanza upya     MIKA,7:7


MUNGU AKUBARIKI UKAWE WAKILI MWAMINIFU
AMEN

2 comments:

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video