Wednesday, April 26, 2017

Kiongozi wa kundi maarufu la Nyimbo
za Asili la Makhirikhiri la nchini
Botswana, Mosesi Malapela a.k.a
Shumba Ratshega, ametangaza kumrudia
Mungu baada ya kuokoka na kuanza
kuhubiri neno la wokovu.
Habari za uhakika kutoka kwa Msemaji
wa Kundi la Makhirikhiri Tanzania,
Livingstone Mkoi zilieleza kuwa, kwa
sasa kiongozi huyo amezaliwa upya
baada ya kuachana na kila kitu cha
kidunia na kuamua kumtumikia Mungu
katika maisha yake.
Livingstone alifunguka: “Ni kweli
Shumba amenieleza kuwa niwaambie
Watanzania kuwa anawaheshimu na
kuwakumbuka kutokana na mapokezi
makubwa waliyompa mwaka 2010
alipofika Tanzania kufanya matamasha
yake yaliyoandaliwa na Kituo cha Radio
Times FM na kumpa mafanikio
makubwa.
“Shumba anasema kuwa katika maisha
yake mapya ya utumishi wa Mungu
amekuwa akiiombea sana Tanzania
pamoja na Rais Dk. John Pombe
Magufuli.
“Kuhusu kuimba anasema ataendelea
kuimba tu na kundi lake halitakufa kwa
vile ule ni utamaduni wao wa asili.”
Mkoi aliongeza: “Tayari mtumishi huyo
ameanza ujenzi wa kanisa lake kubwa
kwenye mji mkuu wa nchi hiyo
(Gaborone) kwa ajili ya kuhubiri Neno la
Mungu.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video