Wednesday, April 26, 2017

BINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA.

Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikiria Rekodi ya kula Chumvi nyingi Duniani kwa sasa.

Mzee Ambilikile Panja ambaye alishuhudia Vitaa kuu zote Mbili za Dunia kwa ukaribu, anakadiriwa kuwa na Umri wa wa zaidi ya miaka 127 leo.

Mkazi huyo wa Kitongoji cha Izyika ambaye kwa sasa haoni wala Kusikia vyema amemsimlia mwandishi wa makala hii kuwa wakati wa Vita ya Maji Maji dhidi Wakoloni alikuwa tayari anachunga mifugo ya Baba yake Marehem Mwanyaluke Panja.

Mzee Ambilikile Panja Kabila Mndali kutoka Tarafa ya  Bundali Ileje anasema, Wakati wa Vita ya Maji Maji "Wazazi wetu walitwambia tukiona Wazungu tuiache mifugo tukimbie kurudi nyumbani" anasema Mzee Panja.

Mzee Panja ambaye kwa sasa hawezi kusimama wala kutembea anasema, Vita ya Kalenga (Mkwawa) haikuwahi kufika kwao Ileje, Isipokuwa Vita ya Pili ya Dunia ilifika mpaka Mbozi.

Anasema Vita ya Hitler, (Vita ya Pili ya Dunia) ilianza Wakati yeye akiwa ameshakimbia kutoka Ileje na kuhamia Mbozi (Kijiji cha Ihanda) baada ya Kupora Mke wa Chifu.  Anasema yeye mwenyewe alishuhudia Mzungu aliyekuwa na Nywele mwili Mzima mithili ya Mnya akiwa amekimbia kujiokoa na Maadui zake. "Tulipo muona huyo Mzungu, tulidhani ni Mnyama kumbe ni Binadamu", anasema kwa Kindali huku akishusha Kicheko hafifu kilichofuatiwa na Kikohozi cha Ukongwe.

Mzee Ambilikile anasema Wakati wa Vita ya Hitler tulilazimika kuchimba Mashimo {Mahandaki} ya kujificha kuleee Lwibhaaa (Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ihanda) <<Handaki hili lipo mpaka sasa eneo hilo.>>

Mzee Panja ambaye mtoto wake wa Kwanza Marehemu Leonard Panja alifariki dunia kutokana na Uzee, mwaka 2014 akiwa na Umri wa miaka 98 anasema Marafiki zake wote, pamoja na Maadui zake wakiwamo Machifu aliokuwa anapingana nao, wote wameshatangulia mbele za haki amebaki pekee yake.

"Mimi nilitoka Kapelekeshi nikaenda kuishi Ibungu Itumba na baadae nikahamia hapa Mbozi. Hapa nilikuja na Mke wangu Mkubwa Agnes Mlawa na Watoto wangu watatu Leonard, Lassary na Pitros pamoja na Zacharia Panja na marehemu Mbonasi Panja (watoto wa ndugu zake)"
anasimulia mzee Panja.

Mzee Ambilikile kwa sasa ni Kikongwe asiyeweza kufanya Chochote bila ya Msaada wa mtu mwingine. Mzee kwa sasa hubebwa au kusukumwa na Kiti cha Magurudumu (Wheel Chair) ambayo humsaidia kwa ajili ya kusogezwa eneo moja hadi jingine.

Kwa sasa Mzee huyu anaishi na Mke wake wa 4 Bi. Atusajigwe Mshani wa Mwisho katika wake zake ambaye naye kwa sasa ni mzee mwenye Umri wa miaka 89 licha ya Kuwa ana umri sawa na Mzaliwa  wa tano wa Mzee Ambilikile Panja.

Aidha, kwa mujibu wa mtoto wa Mwisho wa Mzee Panja ambaye ndiye hutunza takwimu za familia ya Mzee Ambilikile, Ndugu Lawrence A. Panja; Baba yake anadhaniwa alizaliwa mwaka 1890 Katika Kijiji cha Kapelekeshi Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.

Kikongwe huyu hajulikani popote zaidi ya Vijiji vinavyo mzunguka. Hata Serikali ya Wilaya tu haijui kuwa ina Raia wake mwenye Umri mkubwa namna hii.

Ni wajibu wetu kama Nchi kusaidia dunia kumfahamu Babu huyu mwenye Umri Mkubwa kuliko wengine. Ni jukumu la Wandishi na Vyombo mbalimbali pamoja na  Mitandao ya Kijamii kuujulisha Ulimwengu Mtu huyu anayeishi maisha ya mwendo wa Marathon kwa sasa.

Sio kila siku tunafuatilia na kusimulia mambo ya Mataifa ya Nje wakati MUNGU na sisi katupendelea. Kama tumeweza kuuambia ulimwengu Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na sio Kenya basi na hili tunaweza tukiamua.

Mwisho naomba Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini Mashirika ndani na nje ya Nchi, pamoja na Wananchi mbalimbali kujitolea kumsaidia na kumtunza Mzee Panja ambaye kwa Umri wake ni kama Lulu iliyosalia Duniani kwa sasa.

Mwandishi wa Makala hii ni Ndugu Abel Sichembe

Email abelchembe37@gmail.com

Simu No. +255757281046

WhatsApp No. +255655281046

Share, Like, Coment, Re post, Sambaza mpaka iwafikie Guineas World of Record.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video