Ushawahi kuona sherehe ya harusi isiyo na
burudani wala mapochopocho na gharama husika
haizidi dola moja?
Basi wiki hii, Wakenya, Wilson Mutura na Ann
walitumia shilingi mia moja au dola moja tu
kufunga ndoa. Dola yenyewe ilitumika kununua
pete mbili zilizogharimu shilingi mia moja.
Sherehe hiyo tulivu ilifanyika katika mtaa wa
Kasarani, mjini Nairobi.
Walipoona kuwa uhusiano wao ulinoga kwa
kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu na kuwa ni
heri waiweke iwe rasmi, Wilson Mutura na Ann
Mutura walianza safari ya kufunga pingu za
maisha. Lakini safari yenyewe ilikumbwa na
changamoto za kifedha.
Kutokana na mazoea ya sherehe za kifahari
nchini humo, wawili hao walipanga na kupangua
sherehe hiyo kwa sababu hawakuweza
kukusanya kiwango walicholenga cha dola mia
tatu.
Waliofanya harusi ya shilingi 100 za Kenya
wapata usaidizi
Kwa Picha: Harusi 'ghali zaidi' India
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia
mchango, hayakutimizwa.
Hilo liliwafanya waahirishe sherehe hiyo mara
tatu.
"Nilipozungumza na kakangu, aliniambia, kwa nini
nijisumbue ilhali wengi wao hawakuhitaji sherehe
ya harusi?" aliuliza.
Lakini baada ya muda, Bwana harusi, Wilson,
hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi
wake kuhusu uwezo wake.
"Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa.
Mapenzi yetu yalizidi yote," anasema bi Harusi,
Ann.
Ingawa walikuwa na uwezo wa kuishi kwa mtindo
wa 'come we stay' uliomaarufu kwa vijana
wengine ambapo wapenzi wanaishi pamoja bila
kuoana, Wawili hao walikwenda kwa askofu
Jasper Owach kutoka Kanisa la Community
Christian worship centre mjini Nairobi kurasmisha
harusi yao.
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujistiri
kutoka maovu baada ya kupata baraka ya
wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi,"
anasema Wilson.
Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson
aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje
sherehe ikiendelea.
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi
nilipokuwa naendelea na shughuli ya
kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach,
ambaye aliongoza hafla hiyo.
Wilson alirejea na walipokuwa wanatamka kauli
za ndoa, Wilson alitoa pete hizo zilizofungwa kwa
gazeti na wakavikana pete.
Kwa sasa wawili hao, wamewarai vijana
kutozuiwa na uwezo wao wa kifedha na hivyo
basi kuhalalisha mapenzi yao kupitia ndoa.
Marehemu aongezwa kwenye picha za harusi
Kutokana na hatua yao, wawili hao, wamelipiwa
fungate na kupewa zawadi na Wakenya
waliovutiwa na ndoa hiyo ya dola moja.
Bila kutarajia, mwishowe harusi yao imekuwa ya
'kifahari'.
Monday, January 30, 2017
- 7:23 AM
- Unknown
- News
- No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment