Tuesday, February 21, 2017

JESHI la polisi Mkoani Mbeya,
linamshikilia mfanyabiashara
maarufu Jijini Mbeya, Steven
Samweli maarufu kwa jina la
MARANATHA, kwa tuhuma za
kujihusisha na biashara za
dawa za kulevya.
Maranatha ni mfanyabiashara
mkubwa Jijini Mbeya
akijijengea jina kubwa
kutokana na kumiliki
Pharmacy kubwa iliyopo
maeneo ya Kabwe,Jiji Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Dhahiri Kidavashari
alisema kuwa Maranatha,
alikamatwa juzi, kwenye moja
ya duka lake la biashara za
dawa baridi kwa matumizi ya
binadamu.
Alisema, baada ya polisi
kupata taarifa za kuhusishwa
kwa mfanyabiashara huyo na
mtandao wa dawa za kulevya,
liliweka mtego na hatimaye
kufanikiwa kumtia nguvuni na
sasa anahojiwa.
Aidha, kukamatwa kwa
mfanyabiashara huyo,
kunafikisha idadi ya watu
nane wanao tuhumiwa
kujihusisha na uingizaji,
usambazaji na utumiaji wa
dawa za kulevya Mkoa wa
Mbeya, huku watumiaji
wanaoshikiliwa wakiwa ni 23.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video