Kikundi cha muziki wa injili kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania kinachojulikana kama Kihayile Group kimechaguliwa kushishiriki katika tuzo kubwa kabisa za nchini England(London uingeleza) zinazojulikana kama AGMMA 2017 yaani African Gospel Music & Media Awards.
AGMMA ni tuzo kubwa kabisa ambazo hutolewa nchini uingeleza kwaajili ya kutambua mchango mkubwa wa waimbaji wa nyimbo za injili pamoja na wadau wengine wanaotoa mchango mkubwa katika masuala ya injili maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Akizungumza katika uzinduzi wa tuzo hizo mapema mwezi wa January Bwn:Charles Korateng mwanzilishi wa tuzo hizo ambaye pia ni mkurugezi wa 1615 Media ambayo ndio kampuni inayoandaa tuzo hizo,alisema tuzo za mwaka huu azitahusisha tu waimbaji wa muziki wa injili bali zitaenda mbali Zaidi kwa kutambua mchango wa wanablog,Radio na Tv za mtandaoni pamoja na watumishi wa Mungu wa makanisa madogo madoo wanaosukuma injili kwa njia mbalimbali.
Zoezi la kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo limefunguliwa rasmi tar 31/3/2017 na litafungwa rasmi usiku wa tar 21/5/2017 Ambapo ukiachilia mbali Kihayile Group watanzania wengine waliochaguliwa kushiriki tuzo hizo ni Angel Benard pamoja na Christina Shusho na kutoka nchini Kenya ni Mercy Masika.
Wakizungumza na Promover.com Kihayile Group wamesema wanayofuraha kubwa sana kuchaguliwa kushiriki katika tuzo hizo ambapo wamewaomba wanamwanza na watanzania kwa ujumla kuwapigia kura ili waweze kuleta tuzo nyumbani.
Ili kupiga kura katika tuzo hizo utatakiwa kujaza email yako kasha kuchagua unayempigia kura,ambapo unaruhusiwa kupiga kura mara moja tu kwa email moja.Kuwapigia kura moja kwa moja Kihayile group tafadhali fuata link kisha chagua namba 15>> HAPA
Hafla ya utoaji wa Tuzo hiyo itafanyika 3/6/2017 Kwenye ukumbi wa Stratford Circus Centre,jijini London Uingeleza.Kwa maelezo Zaidi fungua>> HAPA
0 comments:
Post a Comment