Tuesday, April 11, 2017



Hayawi Hayawi sasa yamekuwa,lile tukio kubwa
kabisa lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi
hatimaye siku imewadia.
Si kingine bali ni harusi ya mwimbaji mahiri wa
nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania
anayefahamika kwa jila la Madam Frola ambaye
atafanya sherehe kubwa ya harusi tar 30/4/2017
katika ukumbi wa Kishimba Beach iliyopo
mkabala na Rock Beach Garden jijini Mwanza
nchini Tanzania kuanzia majira ya saa 11:00
jioni.
Madam Frola anawakaribisha watu wote kwenye
sherehe hiyo ya aina yake ambapo siku hiyo
itaambatana na uzinduzi wa album yake mpya
kabisa inayokwenda kwa jina la 'WAKATI WAKE'
lakini pia kitabu kipya kinachoitwa 'SIRI ZA
FROLA MBASHA' kitazinduliwa katika sherehe
hiyo.
Kadi za harusi hiyo zinapatikana kwa
Tsh.50,000/=Single na Tsh.70,000/=-Double.Kadi
zinapatikana kwenye hotel ya Belmont Fair
Mount Hotel zamani JB Belmont Hotel,wahi sasa
kadi yako maana kadi ni chache na hazitauzwa
mlangoni siku ya sherehe.
Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya
Tanzania watakuwepo ambapo Madam Frola
ataimba nyimbo zake zote kali Live katika
sherehe hiyo.
Vazi la sherehe hiyo ni rangi nyeupe hivyo basi
unaombwa kuja ukiwa umevalia rangi
nyeupe.Kwa Mawasiliano Zaidi piga simu namba
0758105014/0655105014.Watu wote
mnakaribishwa!
KAMA UNA MATANGAZO UNATAKA YASAMBAZWE KWA BLOG HII
WASILIANA NASI
vijananainjili.blogspot.com
0673008678
0766867600

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video