Share on Twitter
Share on Google
Plus
ISAAC LUHENDE
17:28:00 HABARI
(picha ya maktaba)
Askofu wa kwanza wa
Dayosisi ya Kusini Mashariki
ya Ziwa Victoria, Dr.
Emmanuel Joseph Makala,
ametoa wito kwa wakristo na
watanzania wote kwa ujumla
kupanda mazao
yanayostahimili ukame hasa
katika kipindi hiki ambacho
kumekuwa na uhaba
mkubwa wa mvua
uliosababisha mazao mengi
yaliyopandwa kukauka.
Akizungumza na wakristo
katika ibada iliyofanyika
jana katika kanisa la kiinjili
la kilutheri Tanzania (KKKT)
Usharika wa Ebeneezer
Kanisa Kuu Shinyanga,
askofu huyo amewasihi
kuzitumia mvua
zinazoendelea kunyesha sasa
kwa kupanda mazao
yanayostahimili ukame kama
mtama ili kuweza
kukabiliana na hali ya
upungufu wa chakula nchini.
Pia kutokana na uoto wa asili
kuzidi kupotea kila kukicha,
askofu amewasihi wakristo
kupanda mti angalau mmoja
kwa kila kaya ili kujaribu
kurudishia uoto huo kwani
miti ni chanzo kikubwa cha
kuleta mvua.
Katika ibada hiyo, wakristo
wa dhehebu hilo walifanya
maombi ya kuombea mvua
wakitekeleza agizo
lililotolewa na mkuu wa
kanisa la KKKT Askofu Dr.
Fredrick Shoo.
Sunday, January 29, 2017
- 8:15 PM
- Unknown
- News
- No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment