Monday, February 13, 2017

Na Ibrahim Yassin, Kyela
MKAZI wa Kitongoji cha Njisi,
Kijijiji cha Kilwa, wilayani Kyela,
Tummanye Makula (35) , amekaa
na ujauzito miezi 13 na
kushindwa kujifungua.
Hata hivyo, baada ya maombezi,
alijikuta akijifungua chura na
baadaye mdudu wa ajabu akiwa
na manyoya meusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa
wiki baada ya dada huyo
kumpigia simu Mchungaji wa
Kanisa la Tample Of Prayer For
All Nations Church, Nabii Charles
Mkuvasa wa mjini Kyela akihitaji
kuombewa.
Alicuhukua hatua hiyo  baada ya
kukaa na ujauzito kwa muda wote
huo na kushindwa kujifungua,
licha ya kuzunguka kwa waganga
wa kienyeji.
Akizungumza na MTANZANIA
jana, Tummanye alisema
aliachana na mume wake muda
mrefu na kuamua kuishi na
mama yake mzazi.
Alisema baada ya miaka miwili,
alipata mwanaume mwingine
ambaye alimpa ujauzito huo na
siku zote alikuwa akihudhuria
kliniki katika Hospitali ya Wilaya
Kyela.
Alisema ilipofika miezi tisa,
alipata uchungu siku mbili, lakini
hakujifungua huku madaktari
wakimweleza kuwa njia yake ni
ndogo, licha ya kuwahi kuzaa
mtoto mmoja.
Baada ya siku mbili uchungu huo
ulikata na aliendelea kukaa na
ujauzito wake hadi alipoamua
kunywa dawa na kupiga lamri
kwa waganga wa kienyeji, ingawa
pia  hakufanikiwa lolote, alisema.
Alisema alipokuwa nyumbani
aliambiwa na marafiki zake
aende kwa Nabii Charles
akaombewe kutokana na
kutokuwa na uwezo wa kutembea
na yeye aliomba namba ya simu
na kumpigia.
Alisema Charles alianza
kumuombea na baada ya dakika
tano, alisikia uchungu ikabidi
aingie ndani…muda mfupi
alijifungua chura ambaye
alitoweka katika mazingira ya
utata.
“Nilitoka sebuleni na kumweleza
mchungaji na mama yaangu
nimejifungua chura ambaye
ametoweka katika mazingira ya
utatanishi,” alisema.
Alisema baada ya muda mfupi,
alijisikia uchungu tena na kwenda
chumbani na kujikuta akijifungua
mdudu wa ajabu akiwa na
manyoya kama paka na nywele za
rasta, ikabidi amwite mama yake
na mchungaji.
Mama mzazi wa Tummanye
Makula hakuweza kutaja jina
wala kusema chochote, baada ya
gazeti hili kufika nyumbani
kwake, isipokuwa alikuwa akilia
tu muda wote.
Mkazi wa Kyela, Bonifas Mwalila,
mmoja wa mashuhuda wa tukio
hilo, alisema tukio hilo ni la
kwanza kuliona tangu azaliwe.
Naye Mchungaji Mkuvasa, alisema
baada ya kufika kijijini alimkuta
mama huyo akiwa katika hali
mbaya, kifo kilikuwa kinamwita
lakini kutokana na maombi
alimnusuru.
Diwani wa Kata hiyo, Anna
Makula licha ya kukiri kuwapo
tukio hilo, alisema amekuwa
akishuhudia matukio mengi ya
watu kufika kanisani hapo
wakiwa wamefungwa kamba,
lakini baada ya siku tatu alikuwa
akishangaa wakirudi makwao
wakiwa wazima.
Chanzo:Mtanzania

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video