Wednesday, April 26, 2017

BINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA.

Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikiria Rekodi ya kula Chumvi nyingi Duniani kwa sasa.

Mzee Ambilikile Panja ambaye alishuhudia Vitaa kuu zote Mbili za Dunia kwa ukaribu, anakadiriwa kuwa na Umri wa wa zaidi ya miaka 127 leo.

Mkazi huyo wa Kitongoji cha Izyika ambaye kwa sasa haoni wala Kusikia vyema amemsimlia mwandishi wa makala hii kuwa wakati wa Vita ya Maji Maji dhidi Wakoloni alikuwa tayari anachunga mifugo ya Baba yake Marehem Mwanyaluke Panja.

Mzee Ambilikile Panja Kabila Mndali kutoka Tarafa ya  Bundali Ileje anasema, Wakati wa Vita ya Maji Maji "Wazazi wetu walitwambia tukiona Wazungu tuiache mifugo tukimbie kurudi nyumbani" anasema Mzee Panja.

Mzee Panja ambaye kwa sasa hawezi kusimama wala kutembea anasema, Vita ya Kalenga (Mkwawa) haikuwahi kufika kwao Ileje, Isipokuwa Vita ya Pili ya Dunia ilifika mpaka Mbozi.

Anasema Vita ya Hitler, (Vita ya Pili ya Dunia) ilianza Wakati yeye akiwa ameshakimbia kutoka Ileje na kuhamia Mbozi (Kijiji cha Ihanda) baada ya Kupora Mke wa Chifu.  Anasema yeye mwenyewe alishuhudia Mzungu aliyekuwa na Nywele mwili Mzima mithili ya Mnya akiwa amekimbia kujiokoa na Maadui zake. "Tulipo muona huyo Mzungu, tulidhani ni Mnyama kumbe ni Binadamu", anasema kwa Kindali huku akishusha Kicheko hafifu kilichofuatiwa na Kikohozi cha Ukongwe.

Mzee Ambilikile anasema Wakati wa Vita ya Hitler tulilazimika kuchimba Mashimo {Mahandaki} ya kujificha kuleee Lwibhaaa (Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ihanda) <<Handaki hili lipo mpaka sasa eneo hilo.>>

Mzee Panja ambaye mtoto wake wa Kwanza Marehemu Leonard Panja alifariki dunia kutokana na Uzee, mwaka 2014 akiwa na Umri wa miaka 98 anasema Marafiki zake wote, pamoja na Maadui zake wakiwamo Machifu aliokuwa anapingana nao, wote wameshatangulia mbele za haki amebaki pekee yake.

"Mimi nilitoka Kapelekeshi nikaenda kuishi Ibungu Itumba na baadae nikahamia hapa Mbozi. Hapa nilikuja na Mke wangu Mkubwa Agnes Mlawa na Watoto wangu watatu Leonard, Lassary na Pitros pamoja na Zacharia Panja na marehemu Mbonasi Panja (watoto wa ndugu zake)"
anasimulia mzee Panja.

Mzee Ambilikile kwa sasa ni Kikongwe asiyeweza kufanya Chochote bila ya Msaada wa mtu mwingine. Mzee kwa sasa hubebwa au kusukumwa na Kiti cha Magurudumu (Wheel Chair) ambayo humsaidia kwa ajili ya kusogezwa eneo moja hadi jingine.

Kwa sasa Mzee huyu anaishi na Mke wake wa 4 Bi. Atusajigwe Mshani wa Mwisho katika wake zake ambaye naye kwa sasa ni mzee mwenye Umri wa miaka 89 licha ya Kuwa ana umri sawa na Mzaliwa  wa tano wa Mzee Ambilikile Panja.

Aidha, kwa mujibu wa mtoto wa Mwisho wa Mzee Panja ambaye ndiye hutunza takwimu za familia ya Mzee Ambilikile, Ndugu Lawrence A. Panja; Baba yake anadhaniwa alizaliwa mwaka 1890 Katika Kijiji cha Kapelekeshi Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.

Kikongwe huyu hajulikani popote zaidi ya Vijiji vinavyo mzunguka. Hata Serikali ya Wilaya tu haijui kuwa ina Raia wake mwenye Umri mkubwa namna hii.

Ni wajibu wetu kama Nchi kusaidia dunia kumfahamu Babu huyu mwenye Umri Mkubwa kuliko wengine. Ni jukumu la Wandishi na Vyombo mbalimbali pamoja na  Mitandao ya Kijamii kuujulisha Ulimwengu Mtu huyu anayeishi maisha ya mwendo wa Marathon kwa sasa.

Sio kila siku tunafuatilia na kusimulia mambo ya Mataifa ya Nje wakati MUNGU na sisi katupendelea. Kama tumeweza kuuambia ulimwengu Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na sio Kenya basi na hili tunaweza tukiamua.

Mwisho naomba Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini Mashirika ndani na nje ya Nchi, pamoja na Wananchi mbalimbali kujitolea kumsaidia na kumtunza Mzee Panja ambaye kwa Umri wake ni kama Lulu iliyosalia Duniani kwa sasa.

Mwandishi wa Makala hii ni Ndugu Abel Sichembe

Email abelchembe37@gmail.com

Simu No. +255757281046

WhatsApp No. +255655281046

Share, Like, Coment, Re post, Sambaza mpaka iwafikie Guineas World of Record.




UZINDUZI WA ALBAM HII YA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ALIMAARUFU KWA JINA LA NYELANYELA
Utafanyika tarehe 7/5/2017
ataambatana na waimbaji wengi sana baadhi yao wametajwa hapo juu
AMBATANA NASI MPAKA SIKU YA TUKIO  TUTAWALETEENI HISTORIA FUPI YA MWIMBAJI HUYU

Kiongozi wa kundi maarufu la Nyimbo
za Asili la Makhirikhiri la nchini
Botswana, Mosesi Malapela a.k.a
Shumba Ratshega, ametangaza kumrudia
Mungu baada ya kuokoka na kuanza
kuhubiri neno la wokovu.
Habari za uhakika kutoka kwa Msemaji
wa Kundi la Makhirikhiri Tanzania,
Livingstone Mkoi zilieleza kuwa, kwa
sasa kiongozi huyo amezaliwa upya
baada ya kuachana na kila kitu cha
kidunia na kuamua kumtumikia Mungu
katika maisha yake.
Livingstone alifunguka: “Ni kweli
Shumba amenieleza kuwa niwaambie
Watanzania kuwa anawaheshimu na
kuwakumbuka kutokana na mapokezi
makubwa waliyompa mwaka 2010
alipofika Tanzania kufanya matamasha
yake yaliyoandaliwa na Kituo cha Radio
Times FM na kumpa mafanikio
makubwa.
“Shumba anasema kuwa katika maisha
yake mapya ya utumishi wa Mungu
amekuwa akiiombea sana Tanzania
pamoja na Rais Dk. John Pombe
Magufuli.
“Kuhusu kuimba anasema ataendelea
kuimba tu na kundi lake halitakufa kwa
vile ule ni utamaduni wao wa asili.”
Mkoi aliongeza: “Tayari mtumishi huyo
ameanza ujenzi wa kanisa lake kubwa
kwenye mji mkuu wa nchi hiyo
(Gaborone) kwa ajili ya kuhubiri Neno la
Mungu.

Saturday, April 22, 2017

Thursday, April 20, 2017


                                
                                                          DOWNLOAD MP3

                                                                 DOWNLOAD MP3

Monday, April 17, 2017


                            DOWNLOAD AUDIO GETRUDER MWASILE -VUMILIA


In habari njema zenye furaha teleee
KIJANA WA UDOM
MUSA MPUME (DAKTARI MWIMBAJI)
anatarajia kufanya uzinduzi WA
Album yake ya kwanza tarehe
23/4/2017 jumapili
Mahali tukio litakapofanyika ni
CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)
KITIVO CHA ELIMU (COED)
THEATRE 4
mahali ambapo ibada za USCF hufanyika

HATO KUWA PEKE YAKE ATAAMBATANA NA WAIMBAJI MBALIMBALI WA INJILI DODOMA NA TANZANIA KWA UJUMLA
KAMA VILE
VICTOR KATUMBATU
FRANCIS AMOSI(FRAMO OF GOD)
KIBONA BAND
HOLLY CELEBRATION
DAVID BIKULAKO
nyelanyela mgallah

Na waimbaji wengiii kama walivyotajwa hapo juu katika

USIPANGE KUKOSA SHUGHULI HII MUHIMU SANAAAA

Saturday, April 15, 2017



Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.

Mwasote, ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa injili.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.

Awali, Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Injili.

Hakimu Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili apangiwe shughuli ya kufanya.
15Apr2017

Friday, April 14, 2017


                           DOWNLOAD HAPA AUDIO YA PHILIMON TOKA UDOM


Tuesday, April 11, 2017

Good Morning my people, today is 12 April
2017 and as usual my daily morning I give
big news on the pages of newspapers from
the Beginning and End of the Retort,
Hardnews and Sports to find out what is
going on my man do not let me stay close.







Kikundi cha muziki wa injili kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania kinachojulikana kama Kihayile Group kimechaguliwa kushishiriki katika tuzo kubwa kabisa za nchini England(London uingeleza) zinazojulikana kama AGMMA 2017 yaani African Gospel Music & Media Awards.


AGMMA ni tuzo kubwa kabisa ambazo hutolewa nchini uingeleza kwaajili ya kutambua mchango mkubwa wa waimbaji wa nyimbo za injili pamoja na wadau wengine wanaotoa mchango mkubwa katika masuala ya injili maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Akizungumza katika uzinduzi wa tuzo hizo mapema mwezi wa January Bwn:Charles Korateng  mwanzilishi  wa tuzo hizo ambaye pia ni mkurugezi wa 1615 Media ambayo ndio kampuni inayoandaa tuzo hizo,alisema tuzo za mwaka huu azitahusisha tu waimbaji wa muziki wa injili bali zitaenda mbali Zaidi kwa kutambua mchango wa wanablog,Radio na Tv za mtandaoni pamoja na watumishi wa Mungu wa makanisa madogo madoo wanaosukuma injili kwa njia mbalimbali.

Zoezi la kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo limefunguliwa rasmi tar 31/3/2017 na litafungwa rasmi usiku wa tar 21/5/2017 Ambapo ukiachilia mbali Kihayile Group watanzania wengine waliochaguliwa kushiriki tuzo hizo ni Angel Benard pamoja na Christina Shusho na kutoka nchini Kenya ni Mercy Masika.

Wakizungumza na Promover.com Kihayile Group wamesema wanayofuraha kubwa sana kuchaguliwa kushiriki katika tuzo hizo ambapo wamewaomba wanamwanza na watanzania kwa ujumla kuwapigia kura ili waweze kuleta tuzo nyumbani.

Ili kupiga kura katika tuzo hizo utatakiwa kujaza email yako kasha kuchagua unayempigia kura,ambapo unaruhusiwa kupiga kura mara moja tu kwa email moja.Kuwapigia kura moja kwa moja Kihayile group tafadhali fuata link kisha chagua namba 15>> HAPA


Hafla ya utoaji wa Tuzo hiyo itafanyika 3/6/2017 Kwenye ukumbi wa Stratford Circus Centre,jijini London Uingeleza.Kwa maelezo Zaidi fungua>>  HAPA




Hayawi Hayawi sasa yamekuwa,lile tukio kubwa
kabisa lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi
hatimaye siku imewadia.
Si kingine bali ni harusi ya mwimbaji mahiri wa
nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania
anayefahamika kwa jila la Madam Frola ambaye
atafanya sherehe kubwa ya harusi tar 30/4/2017
katika ukumbi wa Kishimba Beach iliyopo
mkabala na Rock Beach Garden jijini Mwanza
nchini Tanzania kuanzia majira ya saa 11:00
jioni.
Madam Frola anawakaribisha watu wote kwenye
sherehe hiyo ya aina yake ambapo siku hiyo
itaambatana na uzinduzi wa album yake mpya
kabisa inayokwenda kwa jina la 'WAKATI WAKE'
lakini pia kitabu kipya kinachoitwa 'SIRI ZA
FROLA MBASHA' kitazinduliwa katika sherehe
hiyo.
Kadi za harusi hiyo zinapatikana kwa
Tsh.50,000/=Single na Tsh.70,000/=-Double.Kadi
zinapatikana kwenye hotel ya Belmont Fair
Mount Hotel zamani JB Belmont Hotel,wahi sasa
kadi yako maana kadi ni chache na hazitauzwa
mlangoni siku ya sherehe.
Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya
Tanzania watakuwepo ambapo Madam Frola
ataimba nyimbo zake zote kali Live katika
sherehe hiyo.
Vazi la sherehe hiyo ni rangi nyeupe hivyo basi
unaombwa kuja ukiwa umevalia rangi
nyeupe.Kwa Mawasiliano Zaidi piga simu namba
0758105014/0655105014.Watu wote
mnakaribishwa!
KAMA UNA MATANGAZO UNATAKA YASAMBAZWE KWA BLOG HII
WASILIANA NASI
vijananainjili.blogspot.com
0673008678
0766867600

Monday, April 10, 2017

Sunday, April 9, 2017

Saturday, April 8, 2017

 LEO IKIWA NI SIKU YA TAREHE 9 may 2017 jumapili
VIJANA NA INJILI  TUNAWALEA MAGAZETI YOTE YA TANZANIA SOMA UPATE TAARIFA,MATUKIO NA HABARI ILI UPATE MAARIFA NA UFAHAM WA TAIA LAKO NA MATAIFA MENGNE YAKO



Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video