Tuesday, January 31, 2017

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)
limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato
cha nne (CSEE) na QT kwa mwaka
2016. Jumla ya watahiniwa 277,283 ambao ni
sawa na asilimia 70.09 ya watahiniwa
waliofanya mitihani kidato cha nne 2016
wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni 135,859 ambao ni
swa na asilimia 67.06 wakati wavulana
waliofaulu ni 142,424 sawa na asilimia 73.36.
Kwa mwaka 2015, watahiniwa waliofaulu
walikuwa 272,947 sawa na asilimia 67.53.
Ukilinganisha na matokeo ya mwaka huu,
ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.56. Idadi
hii ni ya watainiwa wote, yaani watahiniwa wa
shule na watahiniwa wa kujitegemea.
Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya
kidato cha nne mwaka 2016 –> CSEE 2016
Bonyeza hapa kuweza kuona matokeo ya QT
mwaka 2016 –> (QT) 2016
Wanafunzi 10 Bora Kitaifa
1. Alfred Shauri (Feza Boys)
2. Cynthia Nehemiah Mchechu (St. Francis
Girls)
3. Erick Mamuya (Marian Boys)
4. Jigna Chavda (St. Mary Goreth)
5. Naomi Tundui (Maria Girls)
6. Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
7. Brian Johnson (Marian Boys)
8. Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
9. Ally Hassan Koti (ALCP Kilasara)
10. Emmanuel M. Kajege (Marian Boys)
Wasichana 10 Bora Kitaifa
1. Cynthia Mchechu (St. Francis Girls)
2. Jigna Chavda (Mary Goreti)
3. Naomi Tundui (Maria Girls)
4. Victoria Chang’a (St. Francis Girls)
5. Esther Mndeme (St. Mary’s Mazinde Juu)
6. Christa Edward (St. Francis Girls)
7. Nelda John (Marian Girls)
8. Mariamu Shabani (Kifungilo Girls)
9. Beatrice Mwella (St. Mary’s Mazinde Juu)
10. Rachel Kisasa (Canossa)
Wavulana 10 Bora Kitaifa
1. Alfred Shauri (Feza Boys)
2. Erick Mamuya (Marian Boys)
3. Brian Johnson (Marian Boys)
4. Ally Koti (ALCP Kilasara)
5. Emmanuel Kajege (Marian Boys)
6. John Ng’hwaya (Nyegezi Seminary)
7. Clever Yohana (Living Stone Boys)
8. Desderius Rugabandana (Morning Star)
9. Kennedy Boniface (Feza Boys)
10. Assad Msangi (Feza Boys)
Shule 10 Bora Kitaifa
1. Feza Boys
2. St. Francis Girls
3. Kaizirege Junior
4. Marian Girls
5. Marian Boys
6. St. Aloysius Girls
7. Shamsiye Boys
8. Anwarite Girls
9. Kifungilo Girls
10. Thomas More Machrina
Shule 10 za Mwisho Kitaifa
1. Kitonga
2. Nyeburu
3. Masaki
4. Mbopo
5. Mbondole
6. Somangila Day
7. Dahani
8. Ruponda
9. Makiba
10. Kidete


                          BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

Monday, January 30, 2017

Ushawahi kuona sherehe ya harusi isiyo na
burudani wala mapochopocho na gharama husika
haizidi dola moja?
Basi wiki hii, Wakenya, Wilson Mutura na Ann
walitumia shilingi mia moja au dola moja tu
kufunga ndoa. Dola yenyewe ilitumika kununua
pete mbili zilizogharimu shilingi mia moja.
Sherehe hiyo tulivu ilifanyika katika mtaa wa
Kasarani, mjini Nairobi.
Walipoona kuwa uhusiano wao ulinoga kwa
kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu na kuwa ni
heri waiweke iwe rasmi, Wilson Mutura na Ann
Mutura walianza safari ya kufunga pingu za
maisha. Lakini safari yenyewe ilikumbwa na
changamoto za kifedha.
Kutokana na mazoea ya sherehe za kifahari
nchini humo, wawili hao walipanga na kupangua
sherehe hiyo kwa sababu hawakuweza
kukusanya kiwango walicholenga cha dola mia
tatu.
Waliofanya harusi ya shilingi 100 za Kenya
wapata usaidizi
Kwa Picha: Harusi 'ghali zaidi' India
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia
mchango, hayakutimizwa.
Hilo liliwafanya waahirishe sherehe hiyo mara
tatu.
"Nilipozungumza na kakangu, aliniambia, kwa nini
nijisumbue ilhali wengi wao hawakuhitaji sherehe
ya harusi?" aliuliza.
Lakini baada ya muda, Bwana harusi, Wilson,
hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi
wake kuhusu uwezo wake.
"Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa.
Mapenzi yetu yalizidi yote," anasema bi Harusi,
Ann.
Ingawa walikuwa na uwezo wa kuishi kwa mtindo
wa 'come we stay' uliomaarufu kwa vijana
wengine ambapo wapenzi wanaishi pamoja bila
kuoana, Wawili hao walikwenda kwa askofu
Jasper Owach kutoka Kanisa la Community
Christian worship centre mjini Nairobi kurasmisha
harusi yao.
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujistiri
kutoka maovu baada ya kupata baraka ya
wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi,"
anasema Wilson.
Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson
aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje
sherehe ikiendelea.
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi
nilipokuwa naendelea na shughuli ya
kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach,
ambaye aliongoza hafla hiyo.
Wilson alirejea na walipokuwa wanatamka kauli
za ndoa, Wilson alitoa pete hizo zilizofungwa kwa
gazeti na wakavikana pete.
Kwa sasa wawili hao, wamewarai vijana
kutozuiwa na uwezo wao wa kifedha na hivyo
basi kuhalalisha mapenzi yao kupitia ndoa.
Marehemu aongezwa kwenye picha za harusi
Kutokana na hatua yao, wawili hao, wamelipiwa
fungate na kupewa zawadi na Wakenya
waliovutiwa na ndoa hiyo ya dola moja.
Bila kutarajia, mwishowe harusi yao imekuwa ya
'kifahari'.

Sunday, January 29, 2017

Mtu mmoja amekufa na wengine wanne kujeruhiwa mjini Tukuyu wilayani hapa, baada ya radi kuupiga mti uliokuwa karibu na banda walipojihifadhi wakati mvua ikinyesha.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita karibu na vituo viwili vya mabasi ya daladala na yaendayo mikoani kandokando ya Barabara ya Mbeya-Malawi.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chalya Nyangidu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana na kwamba aliyefariki dunia ni mkazi wa jijini Arusha, Freeman Swai (35) ambaye alifika mkoani hapa kununua ndizi.
Waliojeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Makandana ni Oliva Ipyana (45), Anna Jericho (30), Juliana Francis (32) na Stela Nsile (37) wakazi wa wilayani hapa.
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk Marco Mbata alithibitisha kupokea mwili wa Swai na majeruhi wanne. Alisema baada ya uchunguzi ilibainika, Swai aliungua kwa moto wa radi na kusaidiana na simu iliyokuwa ikitumia kupiga muziki.


Share on Twitter
Share on Google
Plus
 ISAAC LUHENDE 
17:28:00  HABARI
(picha ya maktaba)
Askofu wa kwanza wa
Dayosisi ya Kusini Mashariki
ya Ziwa Victoria, Dr.
Emmanuel Joseph Makala,
ametoa wito kwa wakristo na
watanzania wote kwa ujumla
kupanda mazao
yanayostahimili ukame hasa
katika kipindi hiki ambacho
kumekuwa na uhaba
mkubwa wa mvua
uliosababisha mazao mengi
yaliyopandwa kukauka.
Akizungumza na wakristo
katika ibada iliyofanyika
jana katika kanisa la kiinjili
la kilutheri Tanzania (KKKT)
Usharika wa Ebeneezer
Kanisa Kuu Shinyanga,
askofu huyo amewasihi
kuzitumia mvua
zinazoendelea kunyesha sasa
kwa kupanda mazao
yanayostahimili ukame kama
mtama ili kuweza
kukabiliana na hali ya
upungufu wa chakula nchini.
Pia kutokana na uoto wa asili
kuzidi kupotea kila kukicha,
askofu amewasihi wakristo
kupanda mti angalau mmoja
kwa kila kaya ili kujaribu
kurudishia uoto huo kwani
miti ni chanzo kikubwa cha
kuleta mvua.
Katika ibada hiyo, wakristo
wa dhehebu hilo walifanya
maombi ya kuombea mvua
wakitekeleza agizo
lililotolewa na mkuu wa
kanisa la KKKT Askofu Dr.
Fredrick Shoo.

AJALI:,YA TRENI KIGOMA

Treni inayotoka Kigoma kuja Dar imepata ajali muda huu maeneo ya Mlandizi ikitokea kituo cha Ruvu ambapo Mabehewa zaidi ya 7 yameanguka hakujaripotiwa vifo.

ENDELEA KUTUFUATILIA HAD MWISHO TUTAKULETA TAARIFA KAMA KUNA MAJERUHI AMA WALIOAGA
VIJANA NA INJILI TANZANIA

Friday, January 27, 2017


UZINDUZI UZINDUZI UZINDUZI

KAMA TANGAZO HAPO JUU LINAVYOJIELEZA 
DADA NEEMA CHOMO
MZAWA WA MBOZI MBEYA NA MKAZI WA SUMBAWANGA RUKWA
KWA SASA YUPO DODOMA KIMASOMO
JUMAPILI HII YA TAREHE 29/1/2017
ANAKULETEA 
ALBAM YAKE YA KWANZA INAYOITWA
MKUBALI YESU
ITASINDIKIZWA NA WAIMBAJI MBALIMBALI KAMA ILIVYOELEVYA HAPO JUU KATIKA TANGAZO LA PICHA
kazi hii mara baada ya kuzinduliwa itakuwa ikisambazwa na MWENYEWE 
NEEMA CHOMO 

MAWASILIANO NI
0764876779
TUMA SMS KWA HII NAMBA ,PIGA
MSAADA WOWOTE YUPO TAYARI KUUPOKEA 
wenye malengo ya kuimalisha huduma 
msaada wako ni ujasiri kwake 

UBARIKIWE SANA

Wednesday, January 25, 2017

Sunday, January 22, 2017

                                                               DOWNLOAD MP3

Saturday, January 21, 2017

EAST AFRICAN COMMUNITY
JOB OPPORTUNITIES
The East African Community is a regional
intergovernmental organization comprising the
Republic of Burundi, the Republic of Kenya, the
Republic of Rwanda, the United Republic of
Tanzania, and the Republic of Uganda with its
headquarters in Arusha, Tanzania.
The Treaty for the Establishment of the East
African Community provides that the partner
states agree to establish a Customs Union,
details of which shall be contained in protocol
which shall, inter alia, include Competition. The
protocols on the Establishment of the East
African Community Customs Union and Common
Market regulate Competition matters.
The EAC Competition Act, 2006 established the
East African community Competition in the
Community, consumer welfare and for related
matters.
This is an exciting opportunity for highly
motivated and result-driven professionals who
are citizens of East African Community Partner
states (Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania and
Uganda) to apply for the following positions
1. Registrar, EAC Competition Authority (REF:
EAC/HR/2015-2016/003)
2. Deputy Registrar, Mergers and Acquisitions
(REF:EAC/HR/2015-2016/004)
3. Deputy Registrar, Monopolies and Cartels
(REF: EAC/HR/2015-2016/005)
4. Senior Personal Secretary (REF: EAC/
HR/2015-2016006)
5. Accounts Assistant (REF: EAC/
HR/2015-2016/007)
To download the detailed job descriptions, please
visit the EAC Website: wwwoeac.int link
“Vacancies”.
Terms and Conditions of Service
The post of Registrar is tenable for a contract of
five (5) years none-renewable while the positions
of Deputies Registrar are for a contract of five
(5), cars renewable once. The General staff
positions are tenable for five (5) years renewable
until mandatory retirement age of 60 years
subject satisfactory conduct and performance.
All positions are subject to the application of the
Quota System
Fringe Benefits
All posts offer attractive fringe benefits including
housing allowance, transport allowance,
education allowance, a medical scheme, and
insurance cover.
Education Qualifications
All candidates applying must have qualifications
that are recognized by the relevant national
accreditation body in their respective countries.
This condition is applicable for locally and
internationally attained qualifications.
All professions that require registration with the
specific professional bodies will he expected to
do so in compliance with the requirements of
their respective partner states.
Relevant Working Experience
Internship, training, apprenticeship and clerkship
will not be considered as relevant work
experience.
Equal Opportunity
The EAC is an equal opportunity employer;
therefore, female candidates are particularly
encouraged to apply. EAC will only respond to
those candidates who strictly meet the set
requirements.
How to Apply
Interested candidates who meet the qualification
and experience requirements for this position are
advised to send their applications, detailed
curriculum vitae, photocopies of academic
certificates, names and contact details of three
(3) referees, and a copy of National Identity
Card, or Birth Certificate or Passport showing the
date of birth certificates or passport showing
birth date. Please quote the respective reference
number on both on the application letter and
envelope. For electronic submission, please
quote the respective reference number on the
subject of the email and send to the address
given below.
Applications should be submitted to the address
below not later than Friday, 11 March 2016
PLEASE NOTE
1. You may submit your application either
electronically or in hard copy but not both.
2. Applications which do not: indicate nationality
and age; the reference number; or have an
application letter attached; have certified copies
of their academic degrees and other professional
Certificates; or fail to provide three referees
shall be disqualified.
3. Only qualified candidates will be contacted
Please note that EAC does not require
candidates to pay money for the recruitment
process. All invitations for interviews will be
done in writing
The Director
Executive Selection Division
Deloitte Consulting Limited
10th Floor PPF Tower
Cnr of Ohio Street & Garden Avenue:
P O Box 1559 Dar-es-Salaam, Tanzania
Fax +255(22) 2116379
E-mail: esd@deloitte.co.tz
SHARE THIS
Share on FacebookTweet on TwitterPlus on
Google+

Friday, January 20, 2017

Thursday, January 19, 2017



Wednesday, January 18, 2017

Tuesday, January 17, 2017

Mbeya: Mtoto aliyezikwa jana akutwa chumbani kwake mara baada ya mazishi
Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makabuni hapo .

Sunday, January 15, 2017




Wapendwa nawasalimu katika jina la Bwana wetu mpendwa Yesu kirsto.
Karibu sana katika masomo ambayo utakuwa ukiyakuta katika ukurasa huu, Mungu akubariki sana.
Usisahau pia kumuhita Roho mtakatifu uendelee kutafakari nae somo hili na mengine yatakayo fuata baada hili.
pia ushauri wako ni muhumu sana ili kuboresha huduma hii kwako na MUNGU afanyike baraka katika maisha yako.


SOMO:UWAKILI


UTANGULIZI
Uwakili ni ile hali ya kufanya kazi au wajibu ulio pewa kwa uaminifu bila udanganyifu wowote, kwa maelezo hayo mafupi basi tunaweza kuona kuwa wakili ni mtu aliye chini ya sheria na anaye timiza wajibu wake kwa usahihi bila kufanya udanganyifu wowote.

Luka 12∶42➖44 Inasema., " Ni nani basi aliye wakili mwaminifu mwenye busara ambaye bwana wake atamuweka juu ya utumishi wake wote awape watu posho kwa wakati wake❓ heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta atamkuta anafanya hivyo, kweli atamweka juu ya vitu vyake vyote"

Kanisa leo liko katika hali ya uhitaji na umaskini kwasababu halija gundua ya kwamba siri ya kuondokana na hayo mambo ya uhitaji na umaskini ambao umekuwa wimbo wa taifa yampasa kila mtu kuwa wakili mwaminifu basi hapo ndipo kanisa na taifa kwa ujumla litapona.

Mtu anaweza kujiuliza kuna uhusiano gani kati ya uhitaji na umaskini kwa upande mmoja kwa kutokuwa wakili mwaminifu kwa upande mwingine,
kwa mtu aliye jiuliza swali kama hilo ningependa kumpa jibu kuwa kuna uhusiano mkubwa baina ya mambo haya ukitaka kuondokana na umaskini na uhitaji basi kuwa wakili mwaminifu, hilo ndo jambo la msingi linalo weza kukuvusha.

Inashangaza sana unakuta Wakristo hawatoi zaka kanisani na labda wengine walikuwa wanatoa ila kwasababu zisizo julikana wameacha. Nasema sababu zisizo julikana maana hakuna sababu maharumu kabisa ya kukufanya usimtolee Mungu zaka ikiwa nawewe unajihesabu kuwa ni wakili mwaminifu.
Pia mwingine anaweza kusema mahubiri ya namna hii ni mahubiri ambayo yamelenga baraka za kimwili tu na siyo za rohoni❗❗      Watu wa jinsi hii naomba niwajibu kuwa Injili ya Yesu ni Injili iliyo kamilika, ina uwezo wa kuhudumia roho, nafsi na mwili wa mwanadamu. si kweli kwamba Mungu hujishughulisha na roho zetu pekee na kwamba hajali kuhusu miili.
Mungu wetu utulinda na kututunza na kutufundisha mwili na roho ndipo baraka za Mungu hupitia ndiyo maana tunahitaji kuwa mawakili waaminifu kwake.



BAADA YA UTANGULIZI BASI TURUDI KATIKA SOMO LETU
Katika agano jipya wakili wajibu wake ni kumtolea bwana wake hesabu ama maelezo kamili juu ya jinsi alivyo timiza wajibu wake. kutokana na hili wakili sharti awe ni mtu mwaminifu ndiyo maana Bwana Yesu katika mistari ya LUKA,12∶42➖44 tuliyo isoma hapo juu anauliza ni nani aliye wakili mwaminifu ambaye bwana wake atamkuta akitimiza yale aliyo agizwa na bwana wake hapo bwana wake atakapo rudi?

Wakristo ni mawakili wa Mungu ambao Bwana Yesu amewaweka ili kuangalia mambo ya Mungu hapa duniani hivyo basi wakristo tuna wajibika kutoa hesabu au maelezo kamili kwa mambo yote yale ambayo Mungu ametupa, pia tuna wajibika na kuliangalia kanisa la Bwana maana wakili siyo mwenye mali bali anawajibika kwa wenye mali.

katika  Luka,16:1➖2 
"Tena aliwaambia wanafunzi wake, palikuwa na mtu mmoja tajiri aliye kuwa na wakili wake huyu alishtakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake, akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayo isikia juu yako? toa hesabu ya uwakili wako kwakuwa huwezi kuwa wakili tena."

Na katika 1kor,4:2 imeandikwa
"Hapo tena inayohitajiwa katika mawili ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu"
Hapo ndipo utaona jinsi gani uaminifu wa hali ya juu unahitajika ili uwe wakili mwaminifu.

pia mistari ifuatayo uhusiana na uwakili na uaminifu
  • Luka,12:42 "Bwana akasema ni nani basi aliye wakili mwaminifu mwenye busara ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?"


  • Mwanzo,1:28➖30 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema tazama nimewapa kila mche utoao mbegu ulio juu ya uso wa nchi yote pia na kila mti ambao matunda yake yana mbegu vitakuwa ndivyo chakula chenu, na chakula cha kila mnyama wa nchi na cha kila ndege wa angani na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi chenye uhai, majani yote ya miche ndiyo chakula chenu ikawa hivyo"


  • Wakolosai,1:25 "Ambalo nimefanywa muhudumu wake sawasawa na uwakili wa Mungu niliyo pewa kwa faida yenu nilitimize neno la Mungu"

MAENEO YA UWAKILI
Mungu ametupa maeneo ambayo tunatakiwa kuwa mawakili na waaminifu kwayo, maeneo hayo ni haya yafuatayo:

  1. MUDA:
  2. VIPAWA VYETU NA KARAMA
  3. HAZINA ZETU                                                                                                                                                                   
MUDA: Muda ni mtaji yulio pewa na Mungu ili tuutumie vizuri. naweza kusema kuwa muda ni mtaji muhimu sana kwa mwanadamu zaidi ya mtaji wowote ule, tofauti kati ya maskini na tajiri ipo kati  ya jinsi wanavyo tumia muda kila mmoja wao.
unaweza kuta mtu anasema aah, nipo tu hapa napoteza muda kweli ukiona ume kubari na kukiri kuwa unapoteza muda basi jua upo unajifilisi mwenyewe nivyema usipoteze muda.
Biblia inatufundisha kuutumia muda wetu vyema ZAB.90:12 "Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wa hekima" 
WAEFESO,5:15➖16 "Basi angalieni sana jinsi mnavyo enenda si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima mkiukomboa wakati kwamaana zamani hizi niza wokovu"

Ndugu wekeza muda wako katika vitu na mambo ya maana yanayo dumu milele, kuna mambo yasiyo dumu na kuna mambo yanayo dumu milele, nakushauri wekeza muda wako katika mambo yadumuyo milele.
Mfano wa mambo yadumuyo milele ni:
  • Neno la Mungu, tumia muda wako kusoma na kujifunza neno la Mungu.
  • maombi, tumia muda wako katika maombi
  • kazi ya Mungu,  n.k                                                                                                                                                                      

VIPAWA VYETU NA KARAMA: Hapa nina maana ya vitu binafsi alivyo tupan Mungu wetu mfano, Mwili, Ujuzi, Hekima n.k
USIMWUE FARASI KABLA HAJAFIKISHA UJUMBE, Unaweza kujiuliza kwamba labda nina maana gani kutumia huu msemo, ila maana yangu nikwamba Mungu ametupa vipawa mbalimbali vivyo tuvitumie kuwa mawakili waaminifu katika kipindi Mungu alicho tupa tuishi duniani.
Esta alitumia nafasi aliyokuwa nayo kuwaokoa Israel, pia Yusuph alitumia nafasi aliyo kuwa nayo katika jamii kuwasaidia ndugu zake waliokuwa hawana chakula,
hivyo yatupasa kutambua tumepewa karama kwa kusudi la kuvusha wasio weza kuvuka wenyewe
1korintho,12:4➖7"Basi pana tofauti za karama bali roho ni yeye yule, tena pana tofauti za huduma bali Bwana ni yeye yule, kisha kuna tofauti za kutenda kazi bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote, lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kusaidiana"



HAZINA ZETU:Ndugu uwe maskini au tajiri inabidi kuelewa kanuni za baraka zifuatazo:
  • Kanuni ya kurejeshewa: Luka 6:38,  Mithari,11:24➖31,  Zaburi,41:1➖3
  • Kanuni za kuringanisha kiwango na kipato: Luka,21:1➖4
  • Kanuni ya kutoa kwa moyo wa furaha: 2kor,9:7
  • Kanuni ya kupokea kutoka kwa wengine pale unapo kuwa muhitaji: 2kor,8:15

FEDHA
Naomba ujitahidi twende pamoja kabisa katika kipengele hiki maana tunahitaji kuwa mawakili waaminifu.
Kuna kanuni za Mungu za kukufanya uwe wakili mwaminifu kwa habari ya fedha, nazo ni hizi zifuatazo:
  • Uitunze na kuijari familia yako: 1tim,5:8
  • usiwe mpenda fedha: 1tim,6:10
  • Toa kwa kadri ya ulivyo navyo: 2kor,8:2
  • Utoaji wako utokane na kuongozwa na Roho mtakatifu na uwe una misingi ya Biblia: 2kor,9:7
  • Uwe mkarimu: 1yoh,3:17


ZAKA
BWANA anaagiza tutoe zaka Lawi,27:30ー33  pia tutoe malimbuko, Mithali,3:9
Katika agano jipya Bwana Yesu aliagiza hivi,: "Lakini ole wenu mafarisayo kwakuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga na huku mwaacha mambo ya adili na upendo wa Mungu iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza bila kuyaacha hayo ya pili" LUKA,11:42

KANUNI ZA ZAKA
10% ya mapato yako kabla ya makato yoyote ni zaka ya kumtolea Mungu,  zaka katika agano la kale lilitumika kuwatunza maskini na wahitaji katika Israel Kutoka,23:11 
Agano jipya kuwatunza maskini mdo,4:34一37, Rum,15:26ã…¡27  kuwatunza wahubiri na waalimu galatia,6:6, Luka,10:7

KUMBUKA
Sisi ndiyo tunao amua tuabarikiwe kwa kiasi gani Luka,6:38, mal,3:7─10, mdo,20:35
Unacho panda ndicho unacho vuna Galatia,6:7
Kutumia mali zetu kwa ajiri ya Mungu ni kuwekeza Luka,12:33
Mungu ndiye akupaye nguvu ya kutajilika Kumb,8:18
Mungu ndiye mwenye mali zote na vitu vyote ni vyake Zab.24:1




HITIMISHO
Habakuki,3:2
Ndugu tukumbuke kuwa fadhiri za MUNGU ni nyingi mno hasa pale tunapo tambua kuwa tumejikwaa na kutubu kwa iman basi Mungu hutusamehe na kuturudisha kundini, labda unamwitaji Mungu afufue utoaji wako basi nenda kwa unyenyekevu mbele zake nae ni mwaminifu na mwingi wa rehema atakusikia na kukujibu na kukusamehe pale utakapo kuwa umeteleza na kukupa kibali cha kuanza upya     MIKA,7:7


MUNGU AKUBARIKI UKAWE WAKILI MWAMINIFU
AMEN


                                                              DOWNLOAD MP3
                                                            DOWNLOAD MP3_bwana ni nguvu

Saturday, January 14, 2017

kanisa kathoric lawaandikia ujumbe mzito waumini wa makanisa yoote TAnzania
hii ni kutokana na ukame unayoikumba TANZANIA kwa baadhi ya mikoa
lasisitiza maombi ya kufunga .sala na rehema za MUNGU kama alivyowarehemu wana wa israel
soma barua hii hapa chini

Friday, January 13, 2017



<iframe width="854" height="480" src="https://www.youtube.com/embed/S8DcGIR0H0o" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>

Monday, January 9, 2017

Sunday, January 8, 2017

Saturday, January 7, 2017

https://youtu.be/UQexUPsK1Sc

Tuesday, January 3, 2017

https://youtu.be/F4XHHRcsE_M


http://www.youtube.com/watch?v=RAGqFeZ-msI&feature=youtube_gdata_player

http://www.youtube.com/watch?v=9afvsa66cJ4&feature=youtube_gdata_player

Sunday, January 1, 2017

Powered by Blogger.

Popular Posts

Our Facebook Page

Video